Anjita Child Development Foundation kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, imefanya kikao cha mapitio ya utekelezaji wa PJT–MMMAM kwa tarehe 12 na 13 Agosti, 2025.
Kikao hiki muhimu kilihudhuriwa na wadau mbalimbali, viongozi, na wataalamu kutoka serikalini.
Mgeni rasmi alikuwa Kaimu Mganga Mkuu wa wa Wilaya (DMO), na miongoni mwa washiriki pia alikuwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa.
Maazimio yaliyopitishwa katika kikao:
- Kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma za MMMAM kwa watoto.
- Kutumia majukwaa ya mikutano ya wazazi/jamii kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu ya MMMAM.
- Kutoa mafunzo kwa Maafisa Ustawi wa Jamii (SWOs) juu ya namna ya kuripoti afua za MMMAM.
- Kufanya usajili wa vituo.
- SWOs kubainisha maeneo yatakayofaa kwa ajili ya kuanzisha vituo vya kijamii.




