Anjita, kama mdau wa Ustawi wa Jamii na Mwanachama wa Mwamvuli wa Mtandao wa Malezi Tanzania – TECDEN, imeshiriki kikamilifu katika Wiki ya Ustawi wa Jamii kuanzia 25 hadi 30 Agosti 2025 ikiwa na kauli mbiu “Pata Msada wa Kisaikolojia: Imarisha Afya ya Akili”. Huu ni muda wa kushirikiana, kujifunza, na kuimarisha miradi ya maendeleo endelevu, tukihakikisha jamii yetu inapata fursa bora za ustawi, malezi, na maendeleo ya kila mtu. Anjita Imeendelea kushirikiana na wadamu mbalimbali katika kuchangiza utekelezaji wa program jumuishi ya Taifa ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (JT-MMMMAM).








