News & Updates

Siku ya Mtoto wa Afrika Mkoa wa Pwani

News & Updates

Anjita Child Development Foundation tumeungana na serikali ya Mkoa wa Pwani na wadau wote kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambapo kimkoa imefanyikia katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.

Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Ndg. Change Twamala. Maadhimisho hayo yaliambatana na nyimbo kutoka kwa watoto zenye kubeba ujumbe wa kauli mbiu, risala, hotuba ya mgeni rasmi, mdahalo na ugawaji wa taulo za kike na vifaa vya kusomea kwa watoto wa shule ya msingi kambarage na shule ya sekondari Miembe Saba.

Taasisi ya Anjita inaendelea kujidhatiti katika kuwasaidia watoto na kutoa elimu kwa wazazi, walezi na wadau kwa ujumla kuhusu haki za watoto na elimu ya malezi kwa wanajamii wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

We take processes apart, rethink, rebuild, and deliver them back working smarter than ever before.