
Tanzania inaungana na dunia kuadhimisha Siku ya Familia Duniani tarehe 23-24 Mei 2025 kilele chake kitafanyika Jiji Mwanza.
Kauli mbiu:
“Mtoto Ni Malezi: Msingi wa Familia Bora kwa Taifa Imara.”
Katika kuenzi mchango wa familia katika ukuaji wa mtoto, Kongamano la Malezi Tanzania 2025 litaandaliwa likiwa na lengo la kuhamasisha jamii, wadau na serikali kushirikiana katika kuwekeza kwa watoto.
Matarajio ni familia zinaweka msingi imara wa maadili, afya, elimu, na ustawi kwa kila mtoto.
Tanzania ECD Network kama wadau wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto tutashiriki
Tanzania ya kesho inaanza na familia ya leo.