Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na taasisi ya Anjita na mwandishi Kinara na wadau wa Mkoa tumefanikiwa kufanya kikao cha pili cha kutathmini utekelezaji wa mpango. Zaidi wa wadau 45 walishiriki wakiwepo CSOs, wataalamu ngazi ya serikali, Viongozi wa dini, Dawati la jinsia, Viongozi wa Serikali. Mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa Mh.Rashidi Mchatta.Hususani na hilo taasisi ya TECDEN iliwakilishwa na Ndg. Lazaro Ernest na Michael. Pia tuliweza kupata mwakilishi kutoka Shirika la Children in crossfire kupitia uwepo wa Mtaalamu Mbobezi wa MMMAM ndg. Davis Gisuka
Katika kikao hicho taarifa ya Mkoa iliwezwa wasilishwa kwa Kila idara kuu za kisekta za maeneo ya MMMAM.
Mafanikio makubwa ya kikao ni;
- Uelewa wa PJT-MMMAM kuongezeka kwa wadau na maafisa wa serikali
- Baadhi ya Halmashauri kuingiza shughuli za MMMAM katika mipango na bajeti
- Wadau kutumia fursa zilizpo mf.nyumba za ibada kutoa elimu ya malezi
- Serikali kuubeba mpango wa PJT-MMMAM na kuufanyia kazi
- Waandishi wa habari kuendelea kutoa elimu na kuonesha ushirikiano chanya katika kutoa taarifa za MMMAM katika jamii mf: Chanel 10, Daily News, blog ya Coast Region press club.
Pia kwaajili ya mashirikiano kila idara ya MMMAM iliweza wasilisha taarifa kwakutumia presentation moja iliyoandaliwa kwa pamoja.




