TAASISI ya Anjita Child Development Foundation ya Kibaha imetoa pembejeo za kilimo cha bustani ya mbogamboga zenye thamani ya shilingi milioni 10.8 kwa vikundi vya wakulima wa bustani kwenye Vitongoji vya Mwanabwito na Kidai Kata ya Kikongo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi kuwezesha jamii kupitia kilimo cha bustani na kukabidhi pembejeo kwa vikundi hivyo Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Evelyn Ngwira kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha amesema kuwa mradi huo utakwenda kubadilisha maisha ya jamii kwenye Kata hiyo.
Ngwira amesema kuwa mradi huo wa uwezeshaji jamii ili kujikwamua kiuchumi na kuboresha afya na utasimamiwa na wanajamii wenyewe na watapaswa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo.
“Mnapaswa kulima kwa kuzingatia kalenda ili kupata mazao mazuri ambayo yatakuwa na soko zuri na mradi huu utakuwa endelevu na mtasimamia wenyewe hivyo muwe mfano kwa awamu hii ya kwanza,”amesema Ngwira.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Anjita Janeth Malela amesema kuwa mradi huo umeibuliwa na wananchi wenyewe na wataundesha kwa kusimamiwa na taasisi na wataalamu wa kilimo.
Malela amesema kuwa pembejeo hizo ni ufadhili kutoka Ubalozi wa Marekani ukiwa na lengo la kuongaza kipato kwa familia na kuboresha afya kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kidai Samson Dotto kwa niaba ya diwani wa Kata ya Kikongo amesema kuwa kilimo ni uti wa mgongo kwani wao wanafanya shughuli hizo kando ya Mto Ruvu na utawasaidia kiwasogeza mbele kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.
Naye ofisa kilimo kata ya Kikongo Fortunatus Ng’itu amesema kuwa hiyo ni fursa muhimu kwa wananchi na wanapaswa kuitumia ili kubadili maisha yao.
Moja ya wanufaika wa mradi huo Eliwaza Kingu amesema kuwa wanaishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia mradi huo kwani utawasaidia kuwapunguzia gharama za kununulia pembejeo ambazo ni kubwa.
Kitongoji cha Mwanabwito ni vikundi 3 ambavyo vina watu 9 na kimoja kina watu 10 kwa Kitongoji cha Kidai kuna vikundi 6 kasoro vikundi 2 wapo watu 5 wa tano.
TAASISI ya Anjita Child Development Foundation ya Kibaha imetoa pembejeo za kilimo zenye thamani ya shilingi milioni 10.7 kwa vikundi vya wakulima wa bustani kwenye Vitongoji vya Mwanabwito na Kidai Kata ya Kikongo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi kuwezesha jamii kupitia kilimo cha bustani na kukabidhi pembejeo kwa vikundi hivyo Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Evelyn Ngwira kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha amesema kuwa mradi huo utakwenda kubadilisha maisha ya jamii kwenye Kata hiyo.
Ngwira amesema kuwa mradi huo wa uwezeshaji jamii ili kujikwamua kiuchumi na kuboresha afya na utasimamiwa na wanajamii wenyewe na watapaswa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo.
“Mnapaswa kulima kwa kuzingatia kalenda ili kupata mazao mazuri ambayo yatakuwa na soko zuri na mradi huu utakuwa endelevu na mtasimamia wenyewe hivyo muwe mfano kwa awamu hii ya kwanza,”amesema Ngwira.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Anjita Janeth Malela amesema kuwa mradi huo umeibuliwa na wananchi wenyewe na wataundesha kwa kusimamiwa na taasisi na wataalamu wa kilimo.
Malela amesema kuwa pembejeo hizo ni ufadhili kutoka Ubalozi wa Marekani ukiwa na lengo la kuongaza kipato kwa familia na kuboresha afya kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kidai Samson Dotto kwa niaba ya diwani wa Kata ya Kikongo amesema kuwa kilimo ni uti wa mgongo kwani wao wanafanya shughuli hizo kando ya Mto Ruvu na utawasaidia kiwasogeza mbele kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.
Naye ofisa kilimo kata ya Kikongo Fortunatus Ng’itu amesema kuwa hiyo ni fursa muhimu kwa wananchi na wanapaswa kuitumia ili kubadili maisha yao.
Moja ya wanufaika wa mradi huo Eliwaza Kingu amesema kuwa wanaishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia mradi huo kwani utawasaidia kuwapunguzia gharama za kununulia pembejeo ambazo ni kubwa.
Kitongoji cha Mwanabwito ni vikundi 3 ambavyo vina watu 9 na kimoja kina watu 10 kwa Kitongoji cha Kidai kuna vikundi 6 kina watu 6 kasoro vikundi 2 wapo watu 5 wa tano.