News & Updates

Anjita Child Development Foundation Yashiriki Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani Kitaifa Jijini Mwanza

News & Updates

Taasisi ya Anjita Child Development Foundation imeungana na wadau wengine kushiriki katika maadhimisho ya siku ya familia duniani ambapo kwa Tanzania kitaifa imefanyikia jiji la Mwanza tarehe 24.5.2025. Mgeni rasmi alikuwa Mh. Dkt Doto Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambapo amesisitiza jukumu la kila mzazi na mlezi kutimiza jukumu la kulea na kutunza familia kwaajili ya maslahi mapana ya mtoto na Taifa.

Hususani na hilo Mh. Dkt Doto Biteko alitumia nafasi hiyo katika kuzindua mwongozo wa Taifa wa uanzishaji na uendeshaji wa vikundi vya wazazi vya malezi na matunzo ya mtoto pamoka na mwongozo wa uwezeshaji wa masuala ya malezi kwa viongozi wa dini.

Anjita foundation imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya malezi kwa jamii, kufanya ushawishi na uchechemuzi kwa serikali, wadau wote na jamii kwa ujumla katika kuhamasisha uimarishaji na uwekezaji wa huduma bora za Malezi Makuzi na Maendeleo ya Mtoto.

#sikuyafamilia2025 #kongamanolamalezi2025 #mtotonimalezi #malezicampaing #mtotokwanza #ecdtanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

We take processes apart, rethink, rebuild, and deliver them back working smarter than ever before.